Simba SC

JAMA..JAMA..KWA MAVITU YA HUYU PAPE SAKHO..MSIMU UJAO LITAKUFA JITU HUKO

admin August 16, 2021 12:57 pm


Baada ya kukamilisha usajili kiungo mshambuliaji Pape Ousmane Sakho ameanza mazoezi pamoja na wachezaji wenzake katika kambi inayoendelea nchini Morocco.

Licha ugeni kikosini Sakho ameonyesha kuanza kuzoeana haraka na wenzake kitu mbacho kinaonekana kitakuwa mchango mkubwa kwa timu.

Sakho 24, raia wa Senegal amejiunga moja kwa moja na kikosi kilichopo hapa Morocco akitokea Timu ya Teungueth FC ya nchini kwao.

Sakho ambaye anacheza winga wa kushoto amekuwa mchezaji muhimu wa Teungueth kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho msimu uliopita.

Sakho anakuwa mchezaji wa nne tuliyemsajili msimu huu baada ya Peter Banda, Yusuph Mhilu na Duncan Nyoni.

SIMBA: CHAMA ALIOMBA KUONDOKA, MKWANJA TULIOWAUZA NI MREFU RASMI, ISRAEL MWENDA NI MALI YA SIMBA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply