Yanga SC

YANGA KAMILI GADO KWA MSIMU UJAO, KAZI INAENDELEA

admin August 18, 2021 8:43 am


 YANGA inaendelea na maandalizi kwa ajili ya msimu wa 2021/22 ikiwa ipo nchini Morocco na imewajumuisha wachezaji wake wapya pamoja na wale waliokuwa katika kikosi hicho msimu wa 2020/21.


Miongoni mwa nyota waliopo kambini ni pamoja na Yacouba Songne ambaye ni namba moja kwa utupiaji msimu wa 2020/21 na Zawad Mauya.

Ni mabao 8 alifunga na pasi nne za mabao na kumfanya ahusike kwenye jumla ya mabao 12 kati ya 52 ambayo yalifungwa na timu hiyo.

Kwa wale wachezaji wapya ambao wapo kambini ni pamoja na Jesus Muloko ambaye anatajwa kuwa mbadala wa Tuisila Kisinda ambaye anatajwa kuibukia Morocco. 

Heritier Makambo ambaye aliwahi kucheza Yanga zama za Mwinyi Zahera naye amerejea tena kikosini. 

Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli amesema kuwa kila kitu kinakwenda sawa.

VIDEO: LUIS KUFANYIWA VIPIMO AL AHLY, NABI AKOSHWA NA DJUMA NA MULOKO HII HAPA TIMU MPYA MATAJIRI WA LIGI DARAJA LA KWANZA INAYOTAKA  KUMSAJILI HAMIS TAMBWE

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply