Simba SC
BAADA YA KUPIGWA BEI… KWA MARA YA KWANZA MIQUISSONE AFUNGUKA HAYA KUHUSU SIMBA
Kiungo Mshambuliaji kutoka nchini Msumbiji, Luis Miquissone ameaga rasmi Simba SC.
Miquissone amefanya jambo hilo la kiungwana kwa kuweka ujumbe kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii, akiwalenga wachezaji, mashabiki, wanachama na viongozi wa Simba SC.
“Ndugu Familia ya Simba, Asante kwa kunipenda kama mmoja wenu, Asante kwa Bodi, Mwenyekiti, Mkurugenzi Mtendaji, Uongozi wote, Wafanyakazi na wachezaji wenzangu”.
“Siwezi kusahau mashabiki wetu, mtakuwa siku zote moyoni mwangu. Haikuwa uamuzi rahisi kuondoka Simba, lakini ninahitaji kuchukua hii changamoto inayofuata.” ameandika Miquissone.
Miquissone tayari ameshathibitishwa kuuzwa na Uongozi wa Simba SC, akihusishwa kusajiliwa na Mabingwa wa Soka Barani Afrika Al Ahly ya Misri.
Leave a Reply
You must be logged in to post a comment.