Simba SC

WINGA SIMBA KUIBUKIA RUVU SHOOTING

admin August 25, 2021 3:48 pm


 NYOTA wa zamani wa Simba, Rashid Juma anatajwa kuingia kwenye rada za Ruvu Shooting kwa ajili ya kukipiga hapo kwa msimu wa 2021/22.

Winga huyo anakumbuka bao lake bora alilofunga wakati alipokuwa akikitumikia kikosi cha Polisi Tanzania akiwa nje ya 18 ambapo aliwatungua Namungo FC.

Alisimamishwa ndani ya Polisi Tanzania kutokana na tatizo la utovu wa nidhamu na kwa sasa yupo huru kujiunga na timu nyingine huku akitajwa kuibukia ndani ya Ruvu Shooting.

Nyota huyo amesema kuwa ni kweli miongoni mwa timu ambazo zinahitaji saini yake ni pamoja na Ruvu Shooting hivyo mambo yakikamilika ataweka kila kitu wazi.

“Kwa sasa kuna timu ambazo zinanihitaji ikiwa ni pamoja na RuvuShooting ila kuna mambo ambayo tunakamilisha dili likikamilika kila kitu kitakuwa sawa.

“Kuhusu mkataba wangu na Simba kwa sasa sina mkataba nao,”

Chanzo:Championi

VIDEO: YANGA YATOA TAMKO ISHU YA SAKATA LA MORRISON, JEZI MPYA KALI JOHN BOCCO, MZAWA ALIYEVUNJA UFALME WA WAGENI

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply