kimataifa

BAYERN MUNICH YAPIGA MTU 12

admin August 26, 2021 2:43 am


KLABU ya Bayern Munich yaichapa mabao 12 Bremer SV katika mchezo wa raundi ya kwanza katika mchezo wa raundi ya kwanza ndani ya German Cup.

Mchezo huo uliochezwa Uwanja wa Weserstadion, shujaa alikuwa ni Eric Maxim Choupo-Moting ambaye alitupia mabao manne dk 8,28,35 na 82. Mengine walifunga Jamal Musiala dk 16 na 48, Jan -Luca Warm alijifunga dk 27, Mali Tillman dk 47, Leroy Sane dk 65,Michael Cuisance dk 80, Bound Sarr dk 86 na Corentin Tolisso dk 88.

Katika mchezo huo Bayern Munich walitawala katika kila idara ambapo kwa upande wa mashuti yaliyoelekea langoni walipiga 37 huku wapinzani wao wakipiga mashuti 7 na katika mashuti hayo 37, 21 yalilenga lango na wapinzani wao Bremer SV ni shuti moja lililenga lango.

Umiliki wa mpira ilikuwa ni aslimia 68 kwa Bayern Munich na 32 kwa Bremer SV pasi zilipigwa 612 upande wa Bayern Munich na 287 kwa Bremer SV.

MUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA SPOTI XTRA ALHAMISI SIMBA KAZINI TENA LEO MOROCCO

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply