kimataifa

HARRY KANE BADO YUPOYUPO SANA TOTTENHAM

admin August 26, 2021 3:43 am


HARRY Kane amesema kuwa kwa sasa hataondoka ndani ya kikosi cha Tottenham atabaki kwa msimu mzima baada ya dili lake la kuibukia Manchester City kubuma jumlajumla.

Kane amebakiza mkataba wa miaka mitatu kuendelea kuitumia timu ya Tottenham aliomba kuondoka kwenye kikosi hicho msimu huu ili aweze kutafuta changamoto mpya, lakini amekwama baada ya mazungumzo ya muda mrefu ambayo yalikuwa yakifanyika dhidi ya City kukwama.

Kupitia ukurasa wake wa Twitter, Kane ambaye pia ni nahodha wa timu ya taifa ya England amesema kuwa anafurahi kubaki hapo na atatumia nguvu zake nyingi katika kuipa mafanikio timu hiyo kwa kushirikiana na wachezaji wenzake.

Kwa upande wa Kocha Mkuu wa timu hiyo Nuno Espirito Santo amesema kuwa hiyo ni habari njema na kubwa kwa kila mtu kwa kuwa Kane ameamua kubaki katika kikosi hicho na ana matumaini watafanya vizuri katika mashindano ambayo watashiriki.

“Ni habari kubwa kwa kila mtu kusikia kwamba Kane anabaki, tutafanya vizuri na tutafanya naye kazi leo tukiwa na uhakika wa uwepo wake kesho hilo limeisha,” .

SIMBA KAZINI TENA LEO MOROCCO REAL MADRID WABISHI, WAWEKA MKWANJA WA MAANA KUIPATA SAINI YA MBAPPE

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply