KLABU ya Real Madrid bado haijakata tamaa kuhusu kuipata saini ya mshambuliaji wa PSG, Kylian Mbappe kwa kuamua kuwasilisha bonge moja ya ofa.
Sasa Real Madrid inayoshiriki La Liga imeamua kuwasilisha kiasi cha pauni milioni 137 ambayo ni sawa na bilioni 434.8 kwa fedha ya Tanzania.
Imeelezwa kuwa Rais wa Real Madrid, Florentino Perez ameweka kiasi hicho cha fedha mezani ili kuhakikisha wanampata mshambuliaji huyo kabla ya dirisha la usajili kufungwa.
Mbappe amekataa kusaini mkataba mpya ndani ya PSG na unatarajiwa kumeguka Juni 30 mwakani na usajili wa Ulaya unatarajiwa kufungwa Agosti 31.