kimataifa

PSG YATAJA BEI YA KUMUUZA MBAPPE

admin August 28, 2021 12:43 pm


 KLABU ya Paris Saint Germain, (PSG) imedai kiasi cha pauni 188 m kwa Real Madrid ilikuweza kukamilisha usajili wa Kylian Mbappe imeelezwa hivyo.

 Ilielezwa kuwa Madrid waliandaa kiasi cha pauni 137m kwa ajili ya kukamilisha dili la Mbappe kutua kikosini hapo na PSG inaelezwa wamekataa kiasi hicho.

Mbappe tayari alieleza kuwa anataka kuondoka ndani ya kikosi hicho cha PSG ndiyo maana amekataa kuongeza mkataba mpya.

Ripoti kutoka Ufaransa zinaeleza kuwa kuwa PSG wao wataka kupokea kiasi cha pauni 188m ili kumuachia staa huyo kikosini hapo.

Mkurugenzi wa Soka wa PSG, Leonardo amesema: “Mbappe anataka kuondoka na hilo linaoneka wazi. Kama Madrid wameleta ofa ni wazi anataka kuondoka.

“Hatuwezi kubadili mipango yetu katika wiki ya mwisho kabisa ya usajili. Kama anataka kuondoka hatutamkatalia, ila sisi ndiyo tutaweka mezani kitu gani tunahitaji na mfahamu kuwa bado Monaco wanatudai,” .


PAMOJA NA KUTOLEWA KWA MKOPO..AME AFUNGUKA HAYA KUHUSU SIMBA..AMTUPIA DONGO GOMES VIDEO: MORRISON AMTOLEA UVIVU HAJI MANARA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply