kimataifa

BAADA YA KICHAPO CHA 5 G ARTETA AWASHUKURU MASHABIKI

admin August 29, 2021 4:43 am

 

MIKEL Arteta,  Kocha Mkuu wa Arsenal amesema kuwa wameumia kupoteza mchezo wao wa Ligi Kuu England mbele ya Manchester City wakiwa ugenini katika mchezo uliochezwa Uwanja wa Etihad huku akirudisha shukrani kwa mashabiki na kusikitishwa na kadi nyekundu kwa mchezaji wake.

Ikiwa imecheza jumla ya mechi tatu haijashinda mchezo hata mmoja ndani ya Ligi Kuu England na safu yake ya ushambuliaji haijafunga bao hata moja huku ile ya ulinzi ikiwa imefungwa jumla ya mabao tisa.

Mabao ya City yalifungwa na Iikay Gundogan dk 7, Ferran Torres dk 12 na 84, Gabriel Jesus dk 43 na Rodri dk 53 huku nyota wa Arsenal Granit Xhaka akionyeshwa kadi nyekundu dk 35 jambo ambalo limemkasirisha Arteta kutokana na hali hiyo.

Arteta amesema kuwa ni maumivu ambayo wanapitia kwa kuwa wachezaji wake walipoteza muunganiko baada ya kufungwa mabao matatu jambo lilowafanya waweze kufungwa mabao mengine mawili na aliweza kuwashukuru mashabiki waliojitokeza kuishangilia timu hiyo.

KIPA MPYA YANGA AFIWA NA BABA YAKE..AANDIKA UJUMBE MZITO..AITAJA YANGA.. VIDEO: TAZAMA NAMNA WACHEZAJI YANGA WALIVYOPOKELEWA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply