Home Azam FC AZAM FC KUWEKA KAMBI ZAMBIA

AZAM FC KUWEKA KAMBI ZAMBIA

UONGOZI wa Azam FC umeweka wazi kwamba hesabu zao kwa msimu wa 2021/22 zinaendelea na mpango kwa timu hiyo ni kuweka kambi nchini Zambia kabla ya ligi kuanza.

Timu hiyo inayonolewa na Kocha Mkuu, George Lwandamina ilimaliza msimu ikiwa nafasi ya tatu na ilikusanya pointi 68 baada ya kucheza mechi 34.

Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Abdulkarim Amin amesema kuwa mipango kwa msimu ujao inakwenda sawa na watakwenda nje kuweka kambi.

Lengo la kufanya hivyo ni mazingira mazuri ili waweze kufikia malengo kwa msimu wa 2021/22 ambapo wanashiriki mashindano ya kimataifa katika Kombe la Shirikisho.

“Tunatarajia kwenda nchini Zambia kuweka kambi kwa ajili ya maandalizi ya msimu wa 2021/22, kila kitu kinakwenda sawa.

“Ushiriki wetu katika mashindano ya kimataifa utatufanya nasi tuwe imara kikubwa ni kupewa sapoti kutoka kwa mashabiki na tuna amini tutafanya vizuri,” .

Azam FC kwa sasa inanembo yake mpya ambayo inaonyesha na mwaka wa kuanzishwa timu hiyo ambayo awali ilikuwa inaitwa Mzizima FC.

Ni mwaka 2004 ilianzishwa na imetoa ajira kwa watu zaidi ya 120 huku ikiwa inawalipa wachezaji wake mishara kupitia akaunti zao za benki na sio kwenye dirisha.




 

SOMA NA HII  TUMBO LILIMVURUGA PRINCE DUBE MBELE YA RHINO RANGERS