Home Yanga SC KIMBEMBE: PAMOJA NA KUTAMBULISHWA LEO, KUMBE NABI HAKUMTAKA MAKAMBO

KIMBEMBE: PAMOJA NA KUTAMBULISHWA LEO, KUMBE NABI HAKUMTAKA MAKAMBO


Kocha wa Yanga Nesreddine Nabi amesharejea nchini na soka la bongo inafahamu Mtunisia huyo hakutaka kumsajili Makambo, lakini mabosi wa Yanga tayari walishafika mbali katika kumrejesha.

Kitu rahisi kwa mabosi wa Yanga ni kwamba karibu mashabiki na wanachama wengi waliona ni bora Makambo arejeshwe na wao kuamua kusimamia msimamo huo wa wafuasi wao.

Nabi hakuvutiwa na rekodi ya Makambo akiwa na Horoya kwani alishindwa kutamba na kuamua kusitisha mkataba wake na sasa anarejea Jangwani.

Mapema Makambo aliliamba soka la bongo kwamba anarejea Yanga kuendeleza kazi akianzia palepale alipoishia.

“Mimi Tanzania ni nyumbani kwangu kwa pili na Yanga ni klabu yangu, nikirudi nakuja kuendelea pale nilipoishia,” alisema Makambo wiki moja iliyopita.

SOMA NA HII  JE AZIZ KI ANAONDOKA YANGA...WAKALA WAKE AFUNGUKA MAMELODI WATAJWA...ISHU NZIMA IKO HIVI