Home Yanga SC KIUNGO MPYA YANGA ANAAMINI ATACHEZA KIKOSI CHA KWANZA

KIUNGO MPYA YANGA ANAAMINI ATACHEZA KIKOSI CHA KWANZA


KIUNGO Jimmy Ukonde ambaye alikuwa kwenye majaribio ndani ya kikosi cha Yanga amesema kuwa anaamini kwamba atacheza ndani ya timu hiyo msimu ujao kikosi cha kwanza.


Nyota huyo alikuwa chini ya Kocha Mkuu, Razack Siwa ambaye alipewa jukumu la kusimamia timu hiyo kwenye mashindano ya Kombe la Kagame alicheza mechi tatu na kuonyesha makeke licha ya timu hiyo kutolewa katika hatua ya makundi.

Ukonde alisema kuwa timu ambazo walikutana nazo zilitumia makosa yao kupata ushindi jambo ambalo limewafanya waondelewe mapema jambo ambalo hawakupanga.

β€œImani yangu ni kuona kwamba msimu ujao nitakuwa ndani ya Yanga. Nitacheza kwa sababu ninaweza na kila kitu kinawezekana.

β€œHatukupanga kutoka mapema lakini timu ambazo tulikutana nazo pia zilikuwa zinahitaji matokeo jambo ambalo limefanya tuondolewe kwenye mashindano.

SOMA NA HII  'SOPU' AJILENGESHA TENA KWA MADAKA MISHALE WA YANGA...AFUNGUKA ANAVYOMUOTEAGA..