Home Habari za michezo SIMBA WANAIHOFIA YANGA, ISHU IKO HIVI

SIMBA WANAIHOFIA YANGA, ISHU IKO HIVI

Habari za Michezo

Mchambuzi wa masuala ya soka nchini kupitia Ea Radio, Martin Mwakiposa amesema kuwa mashabiki wa Klabu ya Simba wanahofia mziki wa wapinzani wao Yanga SC kuelekea kwenye mchezo wa dabi ya Kariakoo utakaopigwa Jumapili ijayo, Novemba 5, 2023 katika Dimba la Mkapa.

“Simba wanapata matokeo lakini ile ‘Rhythm’ ya timu inaonekana kupungua na ndio maana ukimsikia Ahmed Ally ameingiwa na hofu kwa sababu timu inapata matokeo lakini akija nje anasikia mashabiki wanavyolalamika.

Mwakiposa amesema hayo kufuatia Meneja Habari wa Klabu ya Simba, Ahmed Ally kutoa kauli kuwa timu pekee ambayo kwa sasa inawapa changamoto kwenye kuwania ubingwa wa Ligi Kuu msimu huu ni yanga kwani Azam ni kama wameshaaga mashindano mapema.

“Ukiitazama Simba kwenye namba inawezekana wakakwambia Yes wako bora, lakini unachokiona kwenye pitch ndio imekuwa shida, na hii ndio ambayo unamsikia Ahmed Ally akijaribu kujirudi akizungumza hivyo akijua kabisa kama ikija ikatokea tofauti na alivyotegemea maana yake kutakuwa na maneno mengi sana.

“Na ndio maana leo hii unaweza kuona akiwamwagia sifa Yanga ni kwa sababu ya kile ambacho ameweza kukiona na kukisikia kwa watu wakizungumza,” Martin Mwakiposa.

SOMA NA HII  JE BALEKE ATAONDOKA SIMBA MWISHO WA MSIMU?...ISHU NZIMA HII HAPA