Home Uncategorized MSHAMBULIAJI MGHANA AKUBALI KUSAINI YANGA

MSHAMBULIAJI MGHANA AKUBALI KUSAINI YANGA


STEVEN Sey, mshambuliaji namba mbili wa Klabu ya Namungo FC amesema kuwa hana tatizo ikiwa Yanga watahitaji saini yake yeye atamwaga wino bila tatizo kwa kuwa kazi yake ni mpira.


Raia huyo wa Ghana mwenye mabao matatu ndani ya Ligi Kuu Bara huku akiwa ametupia matatu kwenye Kombe la Shirikisho Afrika amekuwa akitajwa kuingia anga za Yanga.


Anakumbukwa na vinara hao wa Ligi Kuu Bara kwa bao lake alilomtungua Metacha Mnata walipokutana kwenye mchezo wa ligi Uwanja wa Mkapa wakati wametoshana nguvu kwa kufungana bao 1-1.


 Sey amesema:” Nipo Namungo kwa sasa na ninaskia kwamba Yanga wanahitani saini yangu hilo kwangu naona sawa sina mashaka na uwezo wangu nitasaini ikiwa utaratibu utafuatwa na maisha yataendelea.


“Ukiwa mchezaji huwezi kuchagua kambi ni popote pale na kwa sasa bado nina mkataba na timu yangu ila hakuna kinachoshindikana,” amesema.

SOMA NA HII  TFF YATIA TIMU KIGALI KUIPA SAPOTI AZAM FC