Home Uncategorized TFF YATIA TIMU KIGALI KUIPA SAPOTI AZAM FC

TFF YATIA TIMU KIGALI KUIPA SAPOTI AZAM FC

WALLACE Karia, Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) ameitaka Ttmu ya Azam FC kufanya vema kwenye mchezo wa fainali ya michuano ya Kagame itakayochezwa leo dhidi ya KCCA.

Karia amefika kwenye kambi ya Azam Fc iliyopo nchini Rwanda Hotel ya Hilltop akiongozanna na Kaimu Makamu wa TFF Athuman Nyamlani na Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano Msafiri Mgoyi.

Karia pia alitumia fursa hiyo kufikisha salamu mbalimbali alizopewa na viongozi wa Serikali, akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, ambao wameitakia mkono wa kheri timu hiyo kwa kufanikisha ushindi na hatimaye kupeperusha vema bendera ya Tanzania.

SOMA NA HII  MWANAMICHEZO AZIM DEWJI AZIDI KUTENGAMAA