Home news LWANGA..KAGERE, BOCCO WAZUIA SIMBA DAY…UONGOZI WAFUNGUKA HAYA..

LWANGA..KAGERE, BOCCO WAZUIA SIMBA DAY…UONGOZI WAFUNGUKA HAYA..


MABINGWA wa Tanzania ambao jana walipokea kundi la mwisho la msafara waliokuwa kambini Rabat, Morocco kabla ya leo kuungana tena kwenye mazoezi ya kambi mpya kujiandaa na msimu mpya wa mashindano, wamefichua waliahirisha Simba Day ili kuwapa burudani wanachama na mashabiki, huku ikielezwa kukosekana kwa mastaa kama Taddeo Lwanga, Meddie Kagere na John Bocco ni sababu ya kuahirishwa kwa tamasha hilo kutoka Agosti 28 hadi Septemba 19.

Nyota wa Simba waliopo timu za taifa ni wanane Taifa Stars ambao ni Kennedy Juma, Bocco, Shomary Kapombe, Aisha Manula, Israel Patrick Mwenda, Mzamiru Yassin, Mohamed Hussein ‘Tshabalala’ na Erasto Nyoni wanaoondoka leo kwenda DRC kuvaana na wenyeji Leopards, huku Meddie Kagere ‘MK 14’ akiwa na kikosi cha Rwanda, Taddeo Lwanga akiwa Uganda na Perfect Chikwende yupo timu ya taifa ya Zimbabwe watakaocheza kuwania kufuzu Kombe la Dunia 2022.

Simba ilipanga tamasha kufanyika Agosti 28, badala ya Agosti 8 iliyozoweleka tangu tamasha hilo lilipoasisiwa 2009, huku wakiwachanganya mashabiki kabla ya kutangaza kufanyika Septemba 19, lakini mratibu wa timu amefichua kilichowafanya waahirishe ni kutaka kufunika zaidi kuliko misimu yote.

Akizungumza na gazeti la Mwanaspoti, mratibu huyo, Abbas Suleiman Ally alisema sababu kubwa ya kusogeza mbele ni kutokana na wachezaji wengi kuitwa timu za taifa, hivyo walihisi tamasha lisingenoga kama baadhi ya mastaa wasingekuwepo. “Simba ina wachezaji zaidi ya 10 katika timu za taifa, ikiwamo Taifa Stars sasa kufanya tamasha wakati hawapo sio sawa na ndio maana tukaona ni bora kusogeza mbele, ili wote wawepo na kuwapa rha mashabiki na wanachama wa klabu yetu,” alisema.

“Awali tulishapanga kufanya Agosti 28 na hata uwanja tulishalipia kabisa, ila kukosekana kwa wachezaji wetu wengi tukaona ni bora kusogeza mbele, maana siku hiyo mbali ya jezi tunatambulisha pia wachezaji wetu.”

Habari za ndani zinasema mabosi Msimbazi wamepania kufanya tamasha la aina yake ikiwamo burudani kutoka kwa wasanii wenye majina makubwa, ili kufunika Wiki ya Mwananchi iliyofannyika jana na kusindikizwa na shoo ya Koffi Olomide na wasanii wengine wa nchini.

SOMA NA HII  KUELEKEA MICHUANO YA CAF MSIMU UJAO...NABI KAKUNA KICHWA WEEE..KISHA KAFUNGUKA HILI KUHUSU FEI TOTO....

Timu itakayocheza na Simba kwenye tamasha hilo imeelezwa huenda ikatoka Afrika Kaskazini au Magharibi tofauti na ilivyozoeleka mara nyingi huwa zinatoka Uganda au Zambia na hivi karibuni kuwaleta Asante Kotoko ya Ghana.

Katika hatua nyingine msafara wa mwisho wa Simba uliokuwa Morocco ulitua jana ukiongozwa na Kocha Didier Gomes na kukamilisha kikiosi kilichokuwa kambini Morocco, baada ya juzi kundi la kwanza la wachezaji Ally Salim, Ibrahim Ajibu, Hennock Inonga ‘Varane’, Yusuph Mhilu, Chris Mugalu, Jimmyson Mwanuke na Abdulsamad Kassim wakiongozwa na kocha wa makipa, Mbrazili Milton Nienov na Seleman Matola kutua nchini.