Home Simba SC MCHEZAJI MPYA KUTOKA MALI AKWAMA KUJIUNGA NA SIMBA..SABABU HIZI HAPA

MCHEZAJI MPYA KUTOKA MALI AKWAMA KUJIUNGA NA SIMBA..SABABU HIZI HAPA


MASTAA wanne wapya wa Simba akiwamo beki aliyeporwa kimafia akielekea Jangwani, Henock Inonga ‘Varane’, wameondoka nchini kwenda Morocco kuungana na wenzao waliotangulia kambini ili kujifua kibabe, lakini hilo tizi linaloendelea huko Rabat ni kazi baada ya kazi.

Kocha Didier Gomes ameanza na programu ya gym kurejesha ufiti kwa mastaa wake huku akitumia muda mfupi kukaa nao mmoja mmoja kwa nyakati tofauti kambini kuwaeleza kile anachokitaka kwao na staili zake za ufanyaji kazi. Anataka kila mmoja awajibike kikamilifu kabla hawajarejea Dar es Salaam kukiwasha kwenye michuano ya kimataifa. Wachezaji tisa wa kundi la pili waliondoka jana chini ya Kocha wa Makipa, Milton Nienov aliyetua asubuhi hiyo kutoka Brazili.

Mbali na Varane, wapya wengine waliopaa ni; Yusuph Mhilu, Abdulsamad Kassim na Israel Patrick Mwenda walioungana na wa zamani akiwamo nahodha John Bocco, Chris Mugalu, Ibrahim Ame, Ally Salim na Ibrahim Ajibu tuliyewadokeza mapema ameongezwa mkataba licha ya kujiondoa kambini kabla ya msimu kuisha.

Shuhuda aliyekuwapo Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa JNIA alishuhudia wachezaji hao, ili kutaka kuzuga walipofika walibadilisha jezi za Simba na kuvaa nguo zao za kawaida kisha kupitia mlango wa abiria wanaowasili na kuacha ule wa wanaoondoka ili wasionekane.

Baada ya kuingia ndani nyota hao wanne walikuwa kama hawajuani na hawajatoka mahala pamoja kila mmoja alijitahidi kujificha uso wake akiwa na barakoa pamoja na kofia. Simba imepanga kuwatambulisha wachezaji hao kwenye tamasha lao la Agosti 28.

WANNE WAKWAMA

Katika hatua nyingine nyota wanne wakiwemo watatu wapya walikwama nchini kutokana na sababu tofauti wakashindwa kujiunga na wenzao katika msafara huo wa jana.

Inafahamika wachezaji hao wapya waliokwama ni kiungo mpya kutokea Mali, Saido Kanoute alitua nchini juzi usiku na kushindwa kupata viza, chanjo na kipimo cha covid 19 pamoja na kukamilisha suala lake la usajili.

Wengine Jeremia Kisubi inaelezwa anaweza kuondoka nchini leo kama ilivyo kwa Kanoute, Kibu Denis ambaye suala lake bado na Said Ndemla atakayeungana na Kisubi baada ya kupata hati zao za kusafiria.

SOMA NA HII  MIEZI MIWILI SASA TOKA ASAJILIWE..KIWANGO CHA BANDA CHAWASHTUA SIMBA..WACHUKUA HATUA HIZI