Home Simba SC MRITHI WA MANARA MSIMBAZI AWACHANA WANOISEMA VIBAYA SIMBA..AITAJA AL AHLY

MRITHI WA MANARA MSIMBAZI AWACHANA WANOISEMA VIBAYA SIMBA..AITAJA AL AHLY


Kaimu Afisa Habari wa Klabu Bingwa Tanzania Bara Simba SC Ezekiel Kamwaga amewashukiwa baadhi ya waandishi wa habari nchini Tanzania kwa kuendeleza mpango wa kuisema vibaya klabu hiyo, hasa katika kipindi hiki cha dirisha la usajili.

Kamwaga ameonesha kutokupendezwa na tabia hiyo alipokuwa kwenye mahojiano na Wasafi FM kupitia kipindi cha Sports Arena.

Kamwaga amesema waandishi wa habari wa Tanzania wanapaswa kujenga mfumo wa kusifia mazuri yanayofanywa na klabu ya Simba SC hata kama kuna mapungufu ambayo wamekau wakiyaona kwa maono yao binafsi.

“Nashangaa sana kwa nini waandishi mnaizungumzia sana Simba SC kwa mabaya, klabu yetu imemsajili Sakho kutoka Senegal mpaka leo navyokwambia kwenye nchi yao imekuwa gumzo na wanashangaa kwa nini Sakho aje Simba na asiende Al Ahly ama Ulaya, hatuwasikiii mkijadili hilo” Kamwaga

“Simba pia Imemsajili Dunkan Nyoni pamoja na Peter Banda mpaka leo hii taarifa imekuwa gumzo huko nchini kwao, mimi nazungumza na waandishi wa habari wa Malawi wanasema wanamichezo bado wanashangaa kwa nini wachezaji hao wanakuja Simba hiyo timu ni kubwa kiasi gani” alisema Ezekiel Kamwaga

SOMA NA HII  IMBA, YANGA WAWEKA MIPANGO YAO HII HADHARANI