Home news PAMOJA NA KUWA NA REKODI KALI…HALI YA BOCCO NDANI YA SIMBA YATIA...

PAMOJA NA KUWA NA REKODI KALI…HALI YA BOCCO NDANI YA SIMBA YATIA ‘SIMANZI’…ATIMIZA SIKU 111…


JOHN Bocco ‘Adebayor’ ndiye anayeshikilia rekodi ya kuwa mchezaji aliyefunga bao kwa misimu 13 mfululizo tangu 2008, lakini huwezi kuamini kwamba hadi leo straika huyo wa Simba ametimiza siku 111 bila kucheka na nyavu.

Hadi kufikia sasa Ligi Kuu Bara msimu huu ikiwa raundi ya tano, Bocco bado hajafunga bao lake kuboresha rekodi yake ya kutupia ndani ya misimu 14 mfululizo, kwani alipata nafasi ya kuandika historia walipovaaa na Biashara United mjini Musoma, lakini alipoteza mkwaju wake wa penalti.

Kama hujui ni kwamba mara ya mwisho kwa Bocco kufunga bao lake katika Ligi Kuu Bara ilikuwa Julai 18 mwaka huu wakati ligi ya msimu uliopita ikihitimishwa kwa kufunga bao la penalti dakika za jioni wakati wakiifumua Namungo kwa mabao 4-0 na bao hilo kumfanya awe Mfungaji Bora.

Bao hilo lilimfanya Bocco afikishe mabao 16 na kumpiku nyota mwenzake wa Simba, Chriss Mugalu aliyekuwa na mabao 15 na kwenye mchezo huo dhidi ya Namungo alitupia mawili, lakini dakika nne za nyongeza ilitokea penalti na Bocco kwenda kuipiga na kufunga.

Ukihesabu tangu alipofunga bao hilo la mwisho lililompa tuzo ya ufungaji bora wa msimu uliopita hadi leo wakati ligi ikiwa imesimama kwa wiki mbili ni sawa na siku 111, ingawa kwa namna ligi ilivyo mbichi bado mkali huyo anayo nafasi ya kutupia na kuboresha rekodi yake.

Katika misimu 13 ya kufunga mfululizo akiitumia Azam kwa misimu tisa na minne akiwa na Simba, Bocco amefunga jumla ya mabao 139 na kumfanya awe kinara wa mabao wa muda wote kwa sasa katika ligi ndani ya misimu hiyo.

SOMA NA HII  UKUTA WA YANGA KUTIKISIKA.....NABI ATOA MSIMAMO HUU KUHUSU KUWATUMIA JOB, MWNYETO AU BANGALA...