Home news MTAMBO WA MABAO WASAINI BIASHARA UNITED, BEKI PIA NDANI

MTAMBO WA MABAO WASAINI BIASHARA UNITED, BEKI PIA NDANI


MTAMBO wa mabao ndani ya Biashara United bado upo baada ya kuongeza kandarasi ya miaka miwili kuendelea kuitumikia timu hiyo.

Ni Ramadhan Chombo,’Redondo ambaye alikuwa ni mtengeneza mipango namba moja ndani ya Biashara United. 

Kwa msimu uliopita wa 2020/21 ikiwa imetupia mabao 28 katika mechi 34 alihusika katika mabao 13, alifunga manne na kutoa pasi 9.

Leo Agosti 13 ametangazwa kuongeza mkataba kwa ajili ya msimu wa 2021/22 ambapo zoezi limesimamiwa na Katibu Mkuu Haji Mtete.

Mbali na Redondo pia imemuongezea kandarasi beki Mpapi Nasibu ambaye naye alikuwa na kikosi hicho msimu uliopita na ana uhakika wa kushiriki mashindano ya kimataifa msimu huu.


SOMA NA HII  ODDS ZA USHINDI LEO HII HIZI HAPA...