Home news PANGA LAPITA TANZANIA PRISONS, 16 WAPIGWA CHINI MAZIMA

PANGA LAPITA TANZANIA PRISONS, 16 WAPIGWA CHINI MAZIMA


 WACHEZAJI 16 ndani ya kikosi cha Tanzania Prisons madili yao yamekwishwa na safari ya kuanza kupata changamoto mpya imewadia.

Taarifa ambayo imetolewa leo na Prisons kupitia ukurasa wao wa Instagra immeleza kuwa timu hiyo imeachana na wachezaji 16, baada ya mikataba yao kumalizika na klabu kufikia uamuzi wa kutowaongeza mikataba ya kuendelea nao msimu ujao :-

Wapo wengine ambao wamepata madili mapya hivyo msimu ujao watakuwa kwenye timu zao mpya.

Orodha ambayo imetolewa na Prisons ipo namna hii:-

1.Jeremiah Kisubi.

2.Andrew Ntala. 

3.Prosper Kaini. 

4.Steven Mwaijala. 

5. Nicodem Mwaipaja.

6.Seleman Mangoma. 

7.Hamidu Mohamed. 

8.Francis Joel. 

9.Salumu Bosco.

10.Kassim Mdoe. 

11.Stamili Mbonde.

12.Gasper Mwaipasi.

13.Ramadhan Ibata.

14.Kennedy Kipepe. 

15. Shaban William. 

16. John Sungura.


Hawa hapa wafuatao wako katika mazungumzo na timu ili kujua mustakabali wao 1. Adili Buha 2.Shadrack Thomas 3.Mohamed Mkopi.


SOMA NA HII  KISA USAJILI WA AZIZ KI....MANARA AFUNGUKA HAYA...ADAI YUKO TAYARI KUACHA KAZI YANGA..."MTAJUA UKWELI WOTE"....