Home Yanga SC REKODI ZA MAKIPA WALIOTEMWA MAZIMA YANGA HIZI HAPA

REKODI ZA MAKIPA WALIOTEMWA MAZIMA YANGA HIZI HAPA


MAISHA yanazidi kuendelea kwa sasa ikiwa ni wakati wa usajili ndani ya ardhi ya Bongo kwa ajili ya msimu wa 2021/22.

Mshtuko kwa mashabiki wa Yanga umekuwa ghafla baada ya makipa wake wote wawili kutemwa mazima jambo linalomaanisha kwamba ni sura mpya zitakuwa langoni msimu mpya.

Makipa hao wawili wapo huru kwa sasa baada ya Kocha Mkuu wa timu hiyo Nasreddine Nabi kutokuwa tayari kufanya nao kazi.

Hapa ni rekodi za makipa hao wawili ambao wataanza maisha mapya msimu ujao katika changamoto mpya. Katika mechi 34 ni moja pekee alikaa langoni Ramadhan Kabwili abaye yupo nchini Morocco na kikosi ilikuwa mbele ya Dodoma Jiji:-

Mnata

Metacha Mnata kwa sasa safari yake imewadia akiwa huru kusaini dili jipya timu nyingine baada ya mkataba wake kukamilika.

Ni mechi 23 ambazo alicheza alikuwa ni chaguo namba moja kwa makocha ambao walipita Yanga. Zama za Cedrick Kaze na sasa alimaliza na Nasreddine Nabi ambaye ni muumini mzuri katika suala la nidhamu.

Mnata katika mechi hizo aliyeyusha  dakika 2,070 aliruhusu mabao 13 ya kufungwa.

Anatunguliwa kila baada ya dk 159

Kipa huyo mzawa ana wastani wa kuokota nyavuni bao moja kila baada ya dakika 159 katika mechi ambazo amecheza jambo linaloonyesha kwamba uwezo kwenye mikono yake ni mkubwa.

Amekusanya jumla ya clean sheet 13 na alifungwa katika mechi 10 ndani ya ligi msimu wa 2020/21.

Timu ya Yanga ilimaliza msimu ikiwa nafasi ya pili na msimu ujao wa 2021/22 itashiriki mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika bila uwepo wa  mikono ya nyota huyo.

Hapa alikuwa shujaa

Yanga 1-0 Mbeya City, Kagera Sugar 0-1 Yanga, Mtibwa Sugar 0-1 Yanga, Yanga 3-0 Coastal Union, Yanga 1-0 Polisi Tanzania, Biashara 0-1 Yanga, Gwambina 0-0 Yanga, Azam 0-1 Yanga, Yanga 1-0 JKT Tanzania, Mwadui 0-5 Yanga, Ihefu 0-3 Yanga. 

Namungo 0-0 Yanga na JKT Tanzania 0-2 Yanga.


Alionja joto ya jiwe

SOMA NA HII  KIUNGO MPYA YANGA ANAAMINI ATACHEZA KIKOSI CHA KWANZA

Tanzania Prisons 1-1 Yanga, Mbeya City 1-1 Yanga, Kagera Sugar 3-3 Yanga, Yanga 3-1 Dodoma Jiji, Yanga 2-1 Ruvu Shooting, Yanga 1-1 Simba, Yanga 1-1 Namungo, KMC 1-2 Yanga, Polisi Tanzania 1-1 Yanga, Ruvu Shooting 2-3 Yanga


Utata ulianzia hapa

Juni 17 aliweka mkataba wake rehani baada ya uongozi wa Yanga uliamua kumsimamisha kwa muda usiojulikana kutokana na kitendo chake kisicho cha kiuungwana kwa mashabiki ambao walikuwa wakimzomea kwa kueleza kwamba alifanya uzembe katika kuokoa bao la pili ambalo lilifungwa na David Richard, dakika ya 82.

Mwisho picha inakamilika kwa Metacha kutuongezewa dili jipya na sasa yupo huru kujiunga na timu itakayomhitaji.


Shikalo


Faroukh Shikalo naye safari imemkuta baada ya dili lake la miaka miwili kumeguka.Alicheza jumla ya mechi 10 ambazo ni dakika 900, alikusanya clean sheet nne na alifungwa katika mechi sita.

 Jumla alifungwa mabao 8 akiwa na wastani wa kufungwa bao moja kila baada ya dakika 112.

Hapa alitunguliwa

Yanga 1-1 Prisons, Coastal Union 2-1 Yanga ,Yanga 1-1 KMC, Yanga 3-1 Gwambina, Yanga 0-1 Azam FC ,Yanga 3-2 Mwadui.


Hapa alikuwa shujaa

Yanga 1-0 Mtibwa,Yanga 1-0 Biashara United, Simba 0-1 Yanga, Yanga 2-0 Ihefu.