Home Cecafa Cup YANGA KUTUPA KETE YE MWISHO, YAPANIA KUFUZU NUSU FAINALI

YANGA KUTUPA KETE YE MWISHO, YAPANIA KUFUZU NUSU FAINALI


KIKOSI cha Yanga leo kinatarajiwa kuwa na kazi ya kusaka pointi tatu kwenye mchezo wake wa tatu wa Kombe la Kagame, saa 10:00 jioni ikiwa ni kete ya mwisho kusaka nafasi ya kutinga hatua ya nusu fainali.

 Razack Siwa, Kocha wa Makipa wa timu ya Yanga ambaye kwa sasa ni kiongozi wa benchi hilo kwenye mashindano ya Kagame amesema kuwa watatinga hatua ya nusu fainali kwa namna yoyote ile.

Yanga iliyopo kwenye kundi A na pointi zake 2 itashuka Uwanja wa Mkapa kumenyana na Express wenye pointi 4 ambao ni vinara kwenye kundi hilo.

Akizungumza na Saleh Jembe, Siwa amesema kuwa kushindwa kupata ushindi kwenye mechi zao mbili ambazo walicheza kutawafanya wapambane kwa namna yoyote kushinda mchezo wao wa mwisho.

“Mechi mbili hatujapata ushindi hivyo kwenye mechi yetu ya mwisho hamna namna ni lazima tupambane ili kupata ushindi ambao utatufanya tutinge hatia ya nusu fainali,” amesema Siwa.

 

SOMA NA HII  WAKATI MANULA AKIINUA MIKONO MAPEMA...HIVI NDIVYO DIARRA ANAVYOMTIMULIA VUMBI KWA UBORA...