UONGOZI wa Simba umebainisha kuwa usajili ambao wamefanya ni mzuri kwa kuzingatia umri pamoja na uwezo wa wachezaji huku ukibainisha kuwa ujio wa beki Henock Inonga kutoka Congo ni moja ya sajili bora kwao.
Pia ana uwezo wa kutumia miguu yote miwili na beki wa kiwango cha juu, hakuna mfano wake ni kwa mujibu wa Crestius Magori aliyekuwa CEO wa timu hiyo ila kwa sasa CEO ni Madam Barbara Gonzalez.