Home news BAADA YA KELELE ZA MASHABIKI YANGA KUWA NYINGI…DJUMA AFUNGUKA HAYA..UONGOZI WATOA TAMKO

BAADA YA KELELE ZA MASHABIKI YANGA KUWA NYINGI…DJUMA AFUNGUKA HAYA..UONGOZI WATOA TAMKO


JINSI mashabiki wa Yanga walivyoujaza uwanja kwenye kilele cha Wiki ya Mwananchi, kimesababisha beki wa pembeni wa timu hiyo kushtuka. Lakini amewaambia mashabiki kwamba ; “Tumewasikia,tunafanya kazi.”

Djuma amesajiliwa na Yanga akitokea AS Vita ya Congo na wikiendi iliyopita alionyesha kiwango kikubwa katika mechi ya kirafiki dhidi ya Zanaco, kilichowaviutia mashabiki waliokuwa wakifuatilia mchezo huo ingawa Yanga ilipoteza mabao 2-1.

Alisema anafahamu huu ni msimu wa nne Yanga haijachukua ubingwa wa Ligi Kuu hivyo ni wakati wao sasa kuhakikisha kuwa wanarejesha heshima ya klabu hiyo na anaamini kwa uwezo wa Mungu watafanikiwa.

“Uwanja ni mkubwa na watu wamejaa sana hiyo imeonyesha namna gani wana mapenzi na sisi wachezaji na ndio maana walikuwa wakitushangilia muda wote. Kupoteza ni sehemu tu ya matokeo kwa kuwa timu ndio kwanza imeanza maandalizi ya kujijenga,”alisema Djuma.

Djuma amewataka wanayanga kuwaamini na kuendelea kutoa sapoti katika michezo yote ambayo watacheza ili kuwapa nguvu ya kupambana uwanjani.

Mashabiki walioujaza uwanja siku hiyo walimshangaza Djuma ambaye amekiri kama wachezaji wana kazi ya kupambana kwa jasho na damu kupata matokeo mazuri yatakayowafurahisha mashabiki na wanachama wa klabu hiyo.

Djuma alisema atahakiisha anajituma, anaongeza juhudi na kutobweteka ili aweze kuonyesha kitu ndani ya timu yake mpya ya Yanga na kuisaidia kubeba vikombe kwenye Ligi Kuu Bara na michuano ya kimataifa.

Alisema ametambua Tanzania watu wanapenda mpira hivyo ni somo kwake kama mchezaji kuhakikisha anapambana kadri awezavyo kuipatia mafanikio timu hiyo na kulinda thamani yake iliyowafanya Yanga wamnunue.

UONGOZI WANENA

Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Fredrick Mwakalebela amewatoa hofu mashabiki wa timu hiyo akidai kuwa mambo mazuri yanakuja hivyo wasiingiwe na ubaridi.

“Mashabiki wetu wasife moyo kwani kila mtu ameona uwezo wa wachezaji wetu wapya, walitarajia ushindi kwa sababu ilikuwa ni siku yetu ya furaha lakini haikuwa hivyo kwa hiyo tutegemee mambo makubwa kupitia kikosi chetu kipya kuelekea msimu ujao,” alisema.

Aliongeza kuwa katika siku 10, zilizosalia kabla ya kucheza mchezo wao wa kwanza wa kimataifa dhidi ya River United anaamini kwamba kocha mkuu wa kikosi hicho Mtunisia Nasreddine Nabi atatengeneza muunganiko mzuri kabla ya mchezo huo.

SOMA NA HII  A-Z JINSI YANGA WALIVYOKULA MIWA YA MTIBWA...MAYELE AKOLEZA MOTO..AKABIDHIWA NG'OMBE...

“Ukiangalia wachezaji wetu walikosa muunganiko kwasababu wengi ni wapya,”alisema. Kuhusu kambi ya Morocco Straika mpya wa timu hiyo,Fiston Mayele alisema; “Tulikuwa jandoni kufunzwa jinsi tunavyopaswa kuyapigania mataji kuanzia msimu huu, ngao ya jamii na Ligi ya Mabingwa Afrika.”

Alisema ilikuwa kambi nzuri licha ya kujifunza mbinu za kivita watakazozitumia msimu ujao, walipata muda wa kufahamiana kwasababu ni kikosi kipya.