News

KAZI INAENDELEA, NCHIMBI , MAYELE WAANZA KUCHEKA NA NYAVU

admin September 3, 2021 4:43 am


 KIKOSI cha Yanga kinachonolewa na Kocha Mkuu Nasreddine Nabi kimezidi kujiimarisha kwa ajili ya msimu mpya wa 2021/22.

Baada ya kufanikiwa kufanya tamasha lao la Wiki ya Mwananchi, Agosti 29, Uwanja wa Mkapa nguvu kubwa zimeelekezwa katika msimu mpya.

Awali kambi yao iliyowekwa Morocco ilivunjwa kwa kile ambacho kilielezwa kuwa ni sababu muhimu kwa maslahi mapana ya timu hivyo wanaendelea na kambi wakiwa kwenye kijiji cha Avic Town, Kigamboni.

Kwenye mchezo wao wa kirafiki dhidi ya Zanaco waliruhusu ubao wa Uwanja wa Mkapa kusoma Yanga 1-2 Zanaco jambo ambalo lilibainishwa na Kocha wa Makipa wa Yanga, Razack Siwa kwamba wameona mapungufu watayafanyia kazi.

Pia jana waliweza kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Friends Rangers na kuibuka na ushindi wa mabao 3-1 na watupiaji walikuwa ni Ditram Nchimbi, Fiston Mayele na Yusuph Umamwiko. 

ENGLAND WASHINDA, UBAGUZI WA RANGI WATAWALA MANCHESTER UNITED KUTUMIA MBINU HII KUINASA SAINI YA HAALAND

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply