BONDIA HASSAN Mwakinyo, ametoa shukuran kwa watu mbalimbali kwa ushirikiano ambao wamemuonesha katika maandalizi ya pambano lake na Julius Indogo wa Namibia.
Mwakinyo ametoa shukurani hizo kupitia ukurasa wake wa Twitter ikiwa ni saa chache zimepita tangu, atetee ubingwa wake wa Afrika (ABU) Super Welterweight baada ya kumpiga Julius Indogo, raia wa Namibia raundi ya 4 kwa ‘TKO.’
Pambano hilo limefanyika usiku wa kuamkia Jumamosi tarehe 4 Septemba 2021, katika pambano lililofanyika ukumbi wa Ubungo Plaza, Dar es Salaam.
Mwakinyo ni bondia namba namba 1 Afrika na namba 37 duniani kati ya mabondia 2,050 wa uzani wa super welter.
Katika salamu zake, Mwakinyo amesema hivi;
Awali ya yote nimshukuru Mwenyezi Mungu mana bila yeye hakuna mimi, yeyee ndo mpangaji wa nani ashinde hakika alinichagua mimi kuwa mshindi, pili nishukuru familia yangu mama yangu bi Fatma Hassan na wengine wote kwa ujumla ambao wamesimama na Mimi na kunitia nguvu pale kwenye ugumu,
“Nishukuru management yangu kwa kazi kubwa walionayo juu yangu,mkuu wangu wa mkoa,Serikali kuu, na wizara ya michezo kwa ujumla kwa hakika najivunia,lakini pia sponsors, (wadhamini) wote kama Azam na wengine wa pambano zima toka mwanzo hadi mwisho lakini shukurani ya kipee ni kwako shabiki wangu ambae ndani yako kuna mimi.
“Hakika ninyi mumenipa hadhi na heshima kubwa mimi sio mshindi na nisingefika hapa bila ninyi, lakini kwa ambae pia sio shabiki yangu nakushukuru sana bila kuwepo ninyi msiokuwa mashabiki wangu nisingepata wa kunikosoa pale ninapokosea.
Nawashukuru sana. Ushindi huu ni wa Taifa zima…nitaendelea kusimama kwa ajili ya nchi yangu…nawapenda sana…