kimataifa

RONALDO AMEANZA MATIZI,UWANJANI UHAKIKA JUMANNE

admin September 8, 2021 8:43 am

 


CRISTIANO Ronaldo ingizo jipya ndani ya Manchester United tayari ameanza mazoezi rasmi na timu yake hiyo ya zamani.

Ronaldo anarejea ndani ya kikosi hicho baada ya miaka 12 kupita anapewa nafasi ya kufanya vizuri ndani ya timu hiyo inayoshiriki Ligi Kuu England. 

Taarifa zinaeleza kuwa nyota huyo atakosekana katika mchezo wa wikiendi hii dhidi ya Newcastle hivyo mashabiki huenda hawatamuona nyota wao.

Raia huyo wa Ureno huenda akaanza kuonyesha makeke yake Jumanne kwa kuwa ametakiwa kujiweka karantini kwenye mjengo wake wa kifahari eneo la Cheshire nchini England. 

Nafasi yake kubwa ni kuanza kwenye mchezo dhidi ya Young Boys, Jumanne ijayo ambao utakuwa ni wa Ligi ya Mabingwa Ulaya.

SIMBA AKILI ZOTE KWA YANGA, NGOMA ITAPIGWA KWA MKAPA VIDEO; HAJI MANARA AKARIBISHWA YANGA, SIMBA YAPELEKA MAJINA 31 CAF

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply