news

BALOZI WA TANZANIA AKUTANA NA YANGA NIGERIA, KAZI IPO LEO

admin September 19, 2021 12:43 pm


WAKIWA nchini Nigeria wawakilishi wa Tanzania wamepata nafasi ya kupata nasaha kutoka kwa  Balozi wa Tanzania nchini Nigeria, Dkt. Benson Bana.

Bana alikutana alikutana na viongozi, benchi la ufundi pamoja na wachezaji ambao wapo nchini Nigeria.

Kambi yao ipo mjini Port Harcourt, Nigeria ambapo wanamchezo wa marudio wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Rivers United ikiwa ni hatua ya awali Ligi ya Mabingwa Afrika.

Kiongozi huyo alipata muda wa kuzungumza machache pamoja na kuwapa hamasa wachezaji wa Yanga kuelekea mchezo wa marudiano dhidi ya Rivers United FC.

Kwa mujibu wa nahodha wa Yanga, Bakari Mwamnyeto amesema kuwa wamekubaliana kupambana ili kupata matokeo chanya kwenye mchezo wa leo ambao unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.

Haji Manara, Ofisa Habari wa Yanga amesema kuwa wapo tayari na watapambana kwa jasho jingi kupata ushindi.


TAZAMA HALI ILIVYO NJE NA NDANI YA UWANJA WA MKAPA EMMANUEL OKWI AIBUKA KWENYE SIMBA DAY…MASHABIKI WASHINDWA KUJIZUIA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply