Home news YANGA INA NOMA, YAPIGA NDEGE WATATU KWA JIWE MOJA,BENCHI LA UFUNDI LIMENOGA

YANGA INA NOMA, YAPIGA NDEGE WATATU KWA JIWE MOJA,BENCHI LA UFUNDI LIMENOGA


KUELEKEA kwenye msimu mpya wa 2021/22, mabosi wa Yanga wameamua kuua ndege watatu kwa jiwe moja ili kufikia malengo ambayo wamejiwekea.


Jiwe la kwanza rasmi leo Uongozi wa Klabu ya Yanga umemtambulisha Mkurugenzi wa Maendeleo Soka la Vijana Mwinyi Zahera.

Zahera ana uzoefu na soka la Bongo na amewahi kuinoa timu hiyo kwenye Ligi Kuu Bara pia aliwahi kuwa Mkurugenzi wa Benchi la Ufundi ndani ya kikosi cha Gwambina ya Mwanza ambayo itashiriki Ligi Daraja la Kwanza msimu ujao wa 2021/22.

Pia tayari ameweza kukutana na benchi nzima la ufundi la Yanga na kuzungungumza nao ikiwa ni pamoja na kuelekea mchezo wa kesho wa Kariakoo Dabi dhidi ya Simba, Uwanja wa Mkapa. 



Jiwe lingine la pili ni la kumtambulisha rasmi Kocha Msaidizi Cedric Kaze.

Kaze anakwenda kushirikiana na Nabi kwenye benchi la ufundi na anakumbukwa kwamba ni yeye ambaye alimuachia mikoba Kaze msimu uliopita wa 2021/22 baada ya mabosi wa Yanga kumpiga chini.


Anatarajiwa kuwa sehemu ya benchi la ufundi kesho mbele ya Simba ikiwa vibali vya kazi vitakamilika na hata ikiwa havitakamilika ana muda wa kuzungumza na Nabi kwa kuwa ana uzoefu na soka la Bongo.


Jiwe namba tatu ni neno la Nabi kuelekea kwenye mchezo wa kesho kwamba anahitaji ushindi ili kuwapa furaha mashabiki wa Yanga na anaamini katika uwezo wake.


SOMA NA HII  ODDS ZA FAINAL YA AFCON KWA LEO HIZI HAPA...UKIWEKA HIZI USHINDI NI UHAKIKA...