Home Azam FC AZAM FC KAMILI GADO KUWAVAA WASOMALI

AZAM FC KAMILI GADO KUWAVAA WASOMALI


 UONGOZI wa Azam FC umeweka wazi kuwa upo tayari kwa ajili ya mchezo wa kesho wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Horseed FC ya Somalia.

Mchezo huo ni wa marudio baada ya ule wa awali uliochezwa Uwanja wa Azam Complex kukamilika kwa ubao kusoma Azam FC 3-1 Horseed FC.

Taarifa iliyotolewa na Azam FC kupitia kwa Ofisa Habari Zakaria Thabit imeeleza kuwa:”Vijana wamemaliza salama mazoezi ya mwisho leo asubuhi kabla ya kesho Jumamosi kuivaa Horseed ya Somalia kwenye mchezo wa marudiano wa raundi ya awali ya Kombe la Shirikisho Afrika (CAFCC).

“Mchezo huo utafanyika Uwanja wa Azam Complex saa 10.00 jioni,”.

SOMA NA HII  PAMOJA NA YANGA KUCHEZA ARUSHA LEO...SIMBA WAIPIGA BAO KWA UPANDE WA JEZI...ZAGOMBANIWA KWA NJUGU....