Home Habari za michezo KISA SIMBA…TRY AGAIN AUWA NDEGE WAWILIKWA JIWE MOJA….APEWA SHAVU JIPYA FIFA…

KISA SIMBA…TRY AGAIN AUWA NDEGE WAWILIKWA JIWE MOJA….APEWA SHAVU JIPYA FIFA…

Habari za Simba

Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi Simba, Salim Abdallah ‘Try Again’ yupo Morocco kwa ajili ya mambo mawili makubwa ya kuinufaisha klabu hiyo.

Jambo la kwanza Try Again ni miongoni mwa wawakilishi wachache kutokea Afrika ambao wataudhuria mkutano wa Shirikisho la soka duniani (FIFA), kuhusu mambo mbalimbali ya soka la dunia.

Pia atahudhuria kozi ya uongozi na utawala katika soka inayotolewa na FIFA.

Baada ya hapo Try Again atakuwa na kikao cha Shirikisho la soka Afrika (CAF), kuhusu mambo mbalimbali ya soka la Afrika ikiwemo mashindano ya (Super League), ambayo yataanza hivi karibuni.

Jambo lingine litakalojadiliwa ni masuala ya bajeti nzima na kila timu itakayoshiriki inatakiwa kupata kiasi gani ili kujikimu kabla na baada ya mashindano.

Haraka baada ya kumaliza mambo hayo mawili Try Again atachukua ndege na kutua Guinea kwa ajili ya kuunganisha nguvu na Mratibu wa timu, Abasi Ally kwa ajili ya kuweka mazingira sawa.

Kuna mambo ya msingi Try Again atayaweka sawa Guinea kwa ajili ya kuhakikisha kikosi baada ya kufika siku mbili kabla ya mchezo kukutana na mazingira yote mazuri yapo tayari.

SOMA NA HII  BALAA LA LEO UWANJANI LILIKUWA NAMNA HII, MATOKEO HAYA HAPA