Home news BAADA YA KUPATA DILI KUBWA MOROCCO..FISTON AFUNGUKA HAYA KUHUSU YANGA..

BAADA YA KUPATA DILI KUBWA MOROCCO..FISTON AFUNGUKA HAYA KUHUSU YANGA..


 ALIYEKUWA mshambuliaji wa Yanga, Mrundi,
Fiston Abdulrazack, ametuma salamu za kuwaaga wana Yanga baada ya kusajiliwa na Olympique Club ya Morocco kwa mkataba wa miaka miwili.

Siku chache zilizopita wakati Simba walipoweka kambi Morocco, walicheza mchezo wa kirafiki na klabu hiyo na kutoka sare ya bao 1-1.Timu hiyo inatajwa kuwa kongwe sana nchini humo.

Kwa muda wa miezi sita ambao Fiston aliitumikia Yanga, alifanikiwa kufunga mabao matatu. Akizungumza na Championi Ijumaa, Fiston alisema: “Nawashukuru wana Yanga kwa muda wao na sapoti waliyonionyesha kwa miezi sita, kwa sasa nipo Morocco kwenye timu yangu mpya.

“Nimesaini mkataba wa miaka miwili na nina imani nitakuwa na wakati mzuri nikiwa hapa.”

Nyota huyo alimaliza msimu akiwa ametupia bao moja kwenye Ligi Kuu Bara na moja kwenye Kombe la Shirikisho.

Mshikaji wake Michael Sarpong yeye kwenye ligi alitupia mabao manne na wote kwa sasa hawapo ndanai ya ardhi ya Tanzania baada ya mabosi wao Yanga kutowapa madili mapya.



SOMA NA HII  INGIZO JIPYA YANGA LATUMIA DAKIKA 10 UWANJANI BILA KUGUSA MPIRA