Home Uncategorized MOISE KEAN KWA KUDAIWA KUFANYA SHEREHE NA WANAWAKE ADHABU INAMHUSU

MOISE KEAN KWA KUDAIWA KUFANYA SHEREHE NA WANAWAKE ADHABU INAMHUSU


KLABU ya Everton inayoshiriki Ligi Kuu nchini England imesema kuwa imestushwa na taarifa kuhusu mshambuliaji wao Moise Kean kuvunja sheria ya kumepuka mikusanyiko isiyo ya lazima wakati huu wa kupambana na maambukizi ya Virusi vya Corona.

Taarifa zinaeleza kuwa nyota huyo mwenye miaka 20 aliaandaa sherehe ya siri na kuwakusanya wageni kibao ambao asilimia kubwa inaelezwa kuwa walikuwa ni Wanawake.

Nyota huyo ambaye anatajwa kuwa kwenye ubora wake  msimu huu inaelezwa kuwa alifanya sherehe hiyo kwa siri jambo ambalo haliruhusiwi kwa kipindi hiki cha maambukizi ya Virusi vya Corona.


Taarifa kutoka ndani ya Everton zinaeleza kuwa mabosi hao wameshtushwa na habari hizo hivyo uchunguzi ukikamilika adhabu za kinidhamu zitamhusu nyota huyo kwa kosa la kuvunja utaratibu.

SOMA NA HII  GAMONDI AFUNGUKA HAYA MALIPO UBINGWA PAWEKWA WAZI