Home news INGIZO JIPYA SIMBA LAAHIDI MAKOMBE

INGIZO JIPYA SIMBA LAAHIDI MAKOMBE


 BEKI mpya wa Simba, Mkongomani, Henock Inonga Baka, amewaomba mashabiki wa timu hiyo kumuamini kwa kipindi ambacho atakuwepo hapo, huku akiahidi kutimiza malengo ya timu hiyo ambayo ni kubeba makombe.

Mkongomani huyo amejiunga na Simba msimu huu kwa mkataba wa miaka miwili akitokea DC Motema Pembe ya DR Congo.

Akizungumza na Spoti Xtra, Baka alisema ana mengi ya kuwafanyia Simba, lakini kikubwa anaomba sapoti ya mashabiki huku akifahamu kwamba ni ngumu mchezaji mgeni kuaminika moja kwa moja.

“Nimejiunga na moja ya timu kubwa Afrika ambayo ina wachezaji wengi wakubwa wenye uwezo wa kimataifa.

“Ili mchezaji ufanye vizuri, lazima kwanza uaminike kwa mashabiki, hivyo niwaombe waniamini ili niifanyie makubwa timu yangu mpya ya Simba.

“Nafahamu ushindani uliopo katika timu, hivyo nitahakikisha ninapambana ili kufanikisha malengo ya timu kubeba makombe katika kuelekea msimu ujao,” alisema Baka,”.


SOMA NA HII  ALIYEMALIZANA NA SIMBA APEWA SHAVU LA KITAIFA UGANDA...