Home KMC FC KMC YAPIGA HESABU ZA UBINGWA

KMC YAPIGA HESABU ZA UBINGWA


CHRISTINA Mwagala, Ofisa Habari wa KMC amesema kuwa malengo yao makubwa kwa msimu wa 2021/22 ni kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara ulio mikononi mwa Simba.

Simba ni mabingwa watetezi baada ya kutwaa taji hilo kwa kufikisha jumla ya pointi 83 na walicheza jumla ya mechi 34.

Msimu wa 2020/21 KMC ilimaliza ikiwa nafasi ya tano,ilikusanya jumla ya pointi 48 baada ya kucheza jumla ya mechi 34.

Mwagala ambaye ni moja ya maofisa walio na utayari katika kazi yake amesema kuwa imani kubwa ipo kutokana na uwepo wa mipango ya kuendelea pale ambapo waliishia msimu uliopita na makosa ambayo walifanya msimu uliopita hivyo watayafanyia kazi.

Mwagala amesema hakuna kitu ambacho hakiwezekani hivyo ni suala la muda kufika ligi ianze.

“Hakuna kitu ambacho hakiwezekani, msimu uliopita tulianza vizuri ila kuna makosa ambayo tuliweza kuyafanya hayo benchi la ufundi litayafanyia kazi yasijirudie.

“Kwa msimu mpya tunahitaji kutwaa ubingwa kwani tumefanya usajili mzuri na wachezaji wana kazi ya kutimiza majukumu yao hivyo mashabiki wazidi kutupa sapoti,” .

KMC itafungua ligi kwa kucheza ugenini na mchezo wake wa kwanza itakuwa dhidi ya Polisi Tanzania, Uwanja wa Ushirika, Moshi.

SOMA NA HII  KUELEKEA MECHI YA CAF JUMAMOSI...MASHABIKI YANGA WATAKIWA KUIGA UVAAJI WA MAXI...