Home Habari za michezo FT:- KMC 0-3 YANGA SC…MUDATHIR KAMA KAWA…’MAJINI’ YAMKUMBA GUEDE….

FT:- KMC 0-3 YANGA SC…MUDATHIR KAMA KAWA…’MAJINI’ YAMKUMBA GUEDE….

FT: KMC 0-3 YANGA SC

Bao la mapema zaidi kwa Yanga ndani ya Ligi Kuu Bara limefungwa mzunguko wa pili na Mudathir Yahya Uwanja wa CCM Kirumba dakika ya kwanza.

Ikumbukwe kwamba bao la kwanza kwenye mzunguko wa kwanza lilifungwa na Dickson Job dakika ya 19 Uwanja wa Azam Complex dhidi ya KMC.

Kwenye mchezo wa leo Februari 17 ubao wa Uwanja wa CCM Kirumba wakati ukisoma KMC 0-1 Yanga ni makosa ya safu ya ulinzi kwenye kupeana pasi yaliwaponza na Yanga wakatumia makosa hayo kufunga.

Ni Mudathir Yahya anakuwa nyota wa kwanza kuwainua mashabiki wa Yanga wakiwa ugenini ndani ya Morogoro, Mji kasoro bahari.

SOMA NA HII  WAKATI AKITAJWA KUTUA SIMBA...GEORGE MPOLE KAWASIKILIZA WEE...KISHA AKATAJA HUKU ANAKOPENDA KWENDA...