Home news KUMBE BAO LA MAYELE KWA SIMBA LILIPIKWA NA MATAIFA MATATU

KUMBE BAO LA MAYELE KWA SIMBA LILIPIKWA NA MATAIFA MATATU


 MATAIFA matatu yalihusika kulipika bao pekee la ushindi lililofungwa na nyota wa Yanga, Fiston Mayele ambaye alizima furaha ya Simba kutetea taji la Ngao ya Jamii.

Ilikuwa Septemba 25, Uwanja wa Mkapa ambapo kazi ilianza kwenye miguu ya taifa la Mali ambaye ni kipa Diarra Djigui aliyepiga pasi ndefu iliyokutana na Mtanzania, Farid Mussa.

Utundu wa Mussa katika kuwakwepa mabeki wa Simba wakiongozwa na Pascal Wawa ulimfanya shuti lake likutane na Mayele raia wa Congo ambaye alimtungua Aishi Manula.

Mbali na shuti hilo kumshinda Manula pia mpira huo uliweka rekodi kwa kuguswa zaidi na mguu wa kulia ambapo kuanzia kwa nahodha Bakari Mwanyeto ambaye alimrudisha kipa wake Diarra aliyepiga pasi ndefu wote walitumia mguu wa kulia, hata mtoa pasi pia na mfungaji wote walitumia mguu wa kulia.

Ni bao la kwanza la Mayele kwenye mechi ya ushindani kufunga na alimtungua kipa bora wa msimu uliopita Aishi Manula ambaye alisepa na tuzo ya kipa bora baada ya kukusanya clean sheet 18.

Leo Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi ina kibarua cha kusaka ushindi kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Kagera Sugar.

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Kaitaba ambapo kupitia kwa Ofisa Habari wa Yanga, Haji Manata wamebainisha kuwa wanahitaji pointi tatu muhimu.

SOMA NA HII  WAKATI LEO NI KIVUMBI CHA EUROPA...JAZA MKEKA WAKO KWA ODDS HIZI KISHA UNISHUKURU BAADAYE..