Home kimataifa MESSI ATUPIA KWA MARA YA KWANZA PSG

MESSI ATUPIA KWA MARA YA KWANZA PSG


LIONEL Messi nyota mpya ndani ya kikosi cha Paris Saint-Germain, (PSG) amefunga bao lake la kwanza akiwa na timu hiyo baada ya kuibuka hapo akitokea ndani ya kikosi cha Barcelona.

Ilikuwa ni kwenye Uwanja wa Parc des Princes mbele ya mashabiki 37,350 ambao walihudhuria kutazama mchezo huo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya na PSG ilishinda mabao 2-0 dhidi ya Manchester City.

Ni mabao ya Idrissa Gueye dakika ya 8 na Messi aliweza kupachika bao lake la kwanza dakika ya 74 yamewafanya PSG wawe namba moja katika kundi A huku Manchester City wakiwa nafasi ya tatu.

Ikumbukwe kwamba Messi alishindwa kufurukuta katika mechi tatu ambazo alicheza ndani ya PSG chini ya Kocha Mkuu, Mauricio Pochettino na bao lake hilo linamfanya afikishe jumla ya mabao 673 katika ngazi ya klabu

Kwenye mchezo huo ni Gianluigi Donnaruma kipa wa PSG alichaguliwa kuwa mchezaji bora wa mchezo huo.Pia inakuwa ni kichapo cha kwanza kwa Manchester City kwa hivi karibuni katika Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa kuwa mara ya mwisho kufungwa ilikuwa ni Septemba 2018 mbele ya Lyon walipopoteza kwa kufungwa mabao 2-1.

Pep Guardiola,  Kocha Mkuu wa City amesema kuwa muda mwingine unashinda muda mwingine unapoteza ila kipa wa PSG Donnaruma alifanya kazi yake kwa kuokoa hatari nyingi.


SOMA NA HII  DE GEA ATAONDOKA MANCHESTER UNITED