Home news REKODI ZA MASHUJAA WA SIMBA V YANGA HIZI HAPA

REKODI ZA MASHUJAA WA SIMBA V YANGA HIZI HAPA

WAKATI hesabu za watani wa jadi ni kusepa na taji la Ngao ya Jamii Septemba 25, waliofunga mabao kwenye mechi zilizopita wote wanatazamwa kwa ukaribu ili kuona kama wanaweza kuendelea pale walipoishia.

Ni viungo wawili waliweza kufunga kwa nyakati tofauti, Zawad Mauya wa Yanga alifunga kwenye mchezo wa ligi huku taddeo Lwanga wa Simba yeye alifunga kwenye mchezo wa fainali ya Kombe la Shirikisho.

Kwa msimu uliopita rekodi zao zilikuwa namna hii Spoti Xtra inakuletea ilivyokuwa kwa mashujaa hao wawili:-

Zawad Mauya

Zawad Mauya huyu ni mtibuaji kwani bao lake ambalo aliwatungua Simba kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara ulitia doa rekodi ya Gomes ambaye alikiongoza kikosi hicho kwenye mechi 14 bila kufungwa ila katika mechi ya 15 alionja joto ya kufungwa.

Katika ligi Yanga ikiwa imechea mechi 34 alipata nafasi ya kucheza mechi 18 na alitumia dk 934. Kwenye mabao 52, alifunga bao moja pekee.

Dabi ya kwanza alianzia benchi na alitumia dk 8  timu ilikuwa inanolewa na Cedric Kaze na ubao wa Uwanja wa Mkapa ulisoma Yanga 1-1 Simba, Uwanja wa Mkapa ilikuwa ni Novemba 7.

Jikumbushe mechi alizoyeyusha dakika 90

Mtibwa Sugar 0-1 Yanga, Uwanja wa Jamhuri,dk 90, Morogoro. Gwambina 0-0 Yanga, Novemba 3, Uwanja wa Gwambina Complex, dk 90. Namungo 0-0 Yanga, Uwanja wa Majaliwa, dk 90, Mei 15.Ruvu Shooting 2-3 Yanga, Uwanja wa Mkapa, dk 90. Yanga 3-2 Mwadui FC, Uwanja wa Mkapa, Juni 20 dk 90. Simba 0-1 Yanga, Julai 3, Uwanja wa Mkapa.

Hizi alikwama kuyeyusha dakika 90

Yanga 1-1 Tanzania Prisons dk 75 ilikuwa Septemba 6, Uwanja wa Mkapa. Kagera Sugar 0-1 Yanga, dk 83, Uwanja wa Kaitaba, Septemba 16.Yanga 3-0 Coastal Union, Oktoba 3, dk 45 Uwanja wa Mkapa. Yanga 1-0 Polisi Tanzania, Uwanja wa Uhuru, dk 13.

Biashara United 0-1 Yanga, Uwanja wa Karume, dk 1. Yanga 1-0 JKT Tanzania, Uwanja wa Mkapa dk 36,Novemba 28. Yanga 3-3 Kagera Sugar, Uwanja wa Mkapa dk 45. Polisi Tanzania 1-1 Yanga, Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, dk 17.

SOMA NA HII  MAPINDUZI BALAMA HATMA YAKE MIKONONI MWA KOCHA KUIVAA SIMBA

KMC 1-2 Yanga, Uwanja wa CCM Kirumba, dk 3. JKT Tanzania 0-2 Yanga, Uwanja wa Jamhuri Dodoma, dk 8 na Yanga 2-0 Ihefu, Uwanja wa Mkapa dk 60.

Neno kutoka Yanga

Mkuu wa Kitengo cha Habari ndani ya Yanga, Hassan Bumbuli alisema kuwa wanajipanga kwa ajili ya mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Simba.

Haji Manara, Ofisa Habari wa Yanga aliliambia Spoti Xtra kuwa wanahitaji kuchukua kila kombe ambalo watashiriki.

Lwanga

Taddeo Lwanga aliibuka Simba wakati wa dirisha dogo kuja kuchukua nafasi ya Gerson Fraga ambaye aliumia.Alicheza katika mechi 11 za ligi na mechi 10 alitumia dakika 90 huku mechi moja pekee akitumia dakika 83 ilikuwa Uwanja wa Mkapa wakati ubao ukisoma Simba 0-1 Yanga.

Jumla alitumia dakika 983 hakuweza kufunga bao ndani ya ligi mpaka alipofunga bao pekee la ushindi kwenye Kombe la Shirikisho.

Mechi zake 10 ambazo aliyeyusha dakika 90 ilikuwa namna hii:-Simba 2-2 Azam FC, Uwanja wa Mkapa, Biashara United 0-1 Simba, Uwanja wa Karume, Simba 3-0 JKT Tanzania, Uwanja wa Mkapa, Simba 5-0 Mtibwa Sugar, Uwanja wa Mkapa.

Kagera Sugar 0-2 Simba, Uwanja wa Kaitaba, Namungo 1-3 Simba, Uwanja wa Majaliwa, Ruvu Shooting 0-3 Simba, Uwanja wa CCM Kirumba, Polisi 0-1 Simba, Uwanja wa Kirumba, KMC 0-2 Simba, Uwanja wa Mkapa, Azam FC 1-1 Simba, Uwanja wa Azam Complex.

Neno kutoka Simba

Barbara Gonzalez, Mtendaji Mkuu wa Simba alisema kuwa wanahitaji kushinda kwenye mchezo wao wa Septemba 25 ili waweze kutwaa Ngao ya Jamii.

“Kuna malengo ambayo tumeweka yale ya muda mfupi na muda mrefu. Moja ni kuona tunaweza kushinda mataji yote na tunatabua kwamba tuna mchezo Septemba 25, “.

Kwa upande wa Murtaza Mangungu, Mwenyekiti wa Simba aliliambia Spoti Xtra kuwa wanahitaji ushindi ili wabebe mataji.