Home news SIMBA KUIBUKIA KWA WANAJESHI WA MPAKANI

SIMBA KUIBUKIA KWA WANAJESHI WA MPAKANI


MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Simba kesho wanatarajia kuibukia kwa Wanajeshi wa Mpakani, Biashara United huko Mara.

Simba inayonolewa na Kocha Mkuu, Didier Gomes ina kibarua cha kusaka ushindi kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Biashara United ambao utakuwa ni kwanza kwa msimu wa 2021/22.

 Usiku wa kuamkia leo Septemba 27 kikosi kimewasili jijini Mwanza na kesho asubuhi kinatarajiwa kuibukia Musoma kufanya maandalizi ya mwisho kabla ya mchezo wa kwanza wa Ligi Kuu dhidi ya Biashara United.

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Karume Mara Septemba 28 ambapo timu zote zitapambana kusaka pointi tatu.

Simba ambayo ndani ya uwanja nahodha wao ni John Bocco inaanza ligi ikiwa na maumivu ya kupoteza kwa kufungwa bao 1-0 dhidi ya Yanga kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii.

Mchezo huo ulichezwa Uwanja wa Mkapa ilikuwa Septemba 25 kwa ajili ya ufunguzi wa Ligi Kuu Bara. 



SOMA NA HII  INJINIA HERSI AMWAGA HADHARANI SIRI ZA JINSI YANGA WATAKAVYOBEBA UBINGWA KIUULAINIII...