Home news SIMBA YAPANIA KUFANYA MAKUBWA SEPTEMBA 19 KWA MKAPA

SIMBA YAPANIA KUFANYA MAKUBWA SEPTEMBA 19 KWA MKAPA


 UONGOZI wa Simba umeweka wazi kuwa kuelekea Simba Day, Septemba 19 watafanya mambo mazuri Uwanja wa Mkapa kwa ajili ya mashabiki waliopo Tanzania na nje ya nchi.


Jana ilianza Wiki ya Simba ambayo inatarajiwa kufika tamati rasmi siku ya Jumapili ambapo timu hiyo iliyoweka kambi Arusha itakuwa na mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya TP Mazembe.

Akizungumza na Soka la Bongo, Kaimu Ofisa Habari wa Simba, Ezekiel Kamwaga alisema kuwa mipango inakwenda sawa na wamejipanga kuweza kuwapa mambo mazuri mashabiki wao.

“Maandalizi kiujumla yanakwenda vizuri, kikubwa ni kuona kwamba mashabiki wanaweza kujitokeza kwa wingi kushuhudia mambo mazuri ambayo tumewaandalia kwa ajili yao.

“Tumeona kwamba kumekuwa na muamko mkubwa kutoka kwa mashabiki hilo lipo wazi na wapo wengine ambao watatoka nje ya nchi kwa ajili ya tamasha la Simba, hivyo ni suala la kusubiri kwa wale ambao bado hawajapata tiketi muda ni sasa kwa kuwa tiketi zinapatikana,” alisema.

Septemba 19 mbali na utambulisho wa wachezaji watakaoitumikia timu hiyo kwa msimu wa 2021/22 pia kutakuwa na burudani kutoka kwa wasanii mbalimbali.

SOMA NA HII  MUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA CHAMPIONI JUMATATU