Home news TP MAZEMBE: SIMBA ITAFANYA MAKUBWA KIMATAIFA

TP MAZEMBE: SIMBA ITAFANYA MAKUBWA KIMATAIFA


NYOTA wa TP Mazembe, Rainford Kalaba, ameitabiria makubwa Simba kufanya vizuri kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu huu.


Simba ilipata nafasi ya kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya TP Mazembe Septemba 19, Uwanja wa Mkapa na mashabiki walijitokeza kwa wingi.


Baada ya dakika 90 ubao ulisoma Simba 0-1 TP Mazembe na ni bao la Jean ambaye alifunga kwa mtindo wa Acrobatic baada ya kipa Aish Manula kupambana kutoka nje ya lango.


Akizungumza na Spoti Xtra, Kalaba alisema: “Simba walicheza vizuri na wana timu nzuri pia, naona wakifanya tena vizuri kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika.


“Tatizo lao ni kushindwa kutumia vema nafasi walizotengeneza, hiyo ndiyo kasoro ambayo mimi binafsi nimeiona.”


Kwa sasa kikosi kipo kwenye maadalizi ya msimu mpya wa 2021/22 huku Septemba 25 kikiwa na kazi ya kusaka ushindi mbele ya Yanga.


Utakuwa mchezo wa Ngao ya Jamii na unasubiriwa kwa shauku kubwa na mashabiki pamoja na wadau wa mpira Tanzania na nje ya Tanzania.

SOMA NA HII  CHAMA AKOLEZA 'PILIPILI' ISHU YA MIQUISSONE KURUDI SIMBA...AJIKUTA AKIANIKA KILA KITU HADHARANI...