Home kimataifa USAJILI ULAYA, MAJEMBE HAYA YALILETA MSHTUKO

USAJILI ULAYA, MAJEMBE HAYA YALILETA MSHTUKO


 USAJILI wa Ulaya kwa ajili ya maandalizi ya msimu wa 2021/22 unatajwa kuwa na maajabu kibao kutokana na kutokea mambo ambayo wengi hawakutarajia ikiwa ni pamoja na kusepa kwa Lionel Messi kutoka Barcelona mpaka PSG, Cristiano Ronaldo kutoka Juventus na kurejea Manchester United pamoja na Romelu Lukaku kutoka Inter Milan na kurejea Chelsea.


Mabadiliko hayo pia yanatajwa kuchangiwa na kushuka kwa uchumi kwa timu nyingi duniani pamoja na sheria ambazo zimewekwa katika masuala ya usajili na suala kubwa lililosababisha kuporomoka kwa uchumi ni janga la Corona.

Ilikuwa ngumu kwa wengi kufikiria kwamba Messi angesepa Barcelona kwa kuwa alikuwa tayari kusaini dili la miaka mitano ili abaki ndani ya Uwanja wa Camp Nou na alikuwa tayari kupunguziwa mshahara raia huyo wa Argentina ila mambo yakabuma.

Vilevile Ronaldo yeye dili lake ndani ya Juventus lilikuwa limebakisha miezi 12 kukamilisha miaka minne kwa kuwa alisaini hapo 2018 akitokea Real Madrid lakini msimu uliopita mambo yalikuwa magumu kwake kwa kuwa Juventus ilitolewa katika Ligi ya Mabingwa Ulaya hatua ya 16 bora na hawakutwaa ubingwa wa Seria A alikuwa anatajwa kuibukia Manchester City ila mabosi wa United wakapindua meza na sasa ni mali yao tena.

Pia usajili wa Romelu Lukaku ambaye ni chaguo la Kocha Mkuu, Thomas Tuchel nao ulikuwa ni wa kushtua kwa kuwa awali Lukaku aligoma kurejea hapo na mwisho wa siku ameanza kazi na alifunga katika mchezo wake dhidi ya Arsenal pia mbele ya Liverpool ya Jurgen Klopp nyota huyo alikiwasha.

SOMA NA HII  WAKATI WAKIWA WANASHINDA KWA TABU..MORRISON AKOLEZA 'SHIDA' SIMBA..AFUNGUKA A-Z...