Home Uncategorized PAUL POGBA KUIWAHI MANCHESTER CITY

PAUL POGBA KUIWAHI MANCHESTER CITY


KIUNGO machachari wa timu ya Manchester United, Paul Pogba ana matumaini ya kurejea uwanjani baada ya wiki mbili na inatajwa kuwa atawawahi wapinzani wake Manchester City.
Imeripotiwa kuwa nyota huyo wa mabingwa wa Kombe la Dunia, Ufaransa ana matumaini makubwa ya kujiunga na timu yake hiyo kutokana na mazoezi ambayo anayafanya kwa sasa kumrejesha kwenye uimara.
Pogba ana tibu majeraha ya enka ambayo aliyapata mwaka jana na hajaonekana uwanjani kwa muda mrefu ambapo kwa sasa matumaini yapo baada ya wiki mbili anaweza kurejea.
Kurejea kwakwe mapema kutatoa nafasi kwa Kocha Mkuu wa Manchester United, Ole Gunnar Solskjaer kumtumia kwenye mechi ya dabi dhidi ya Manchester City inayotarajiwa kuchezwa Machi 8 pamoja na ile itakayofuata Machi 15 dhidi ya Tottenham.
Pogba mwenye miaka 26 imekuwa ikitajwa kuwa ana mpango wa kusepa ndani ya kikosi hicho cha United huku Juventus wakipewa chapuo la kuinasa saini yake.
SOMA NA HII  ALIYEELEZWA KUHITAJIKA YANGA APIGWA CHINI KENYA