Home Yanga SC YANGA: KIGOMA TUNAWAFUNGA TENA SIMBA, WAMETUSHINDWA KWA MKAPA

YANGA: KIGOMA TUNAWAFUNGA TENA SIMBA, WAMETUSHINDWA KWA MKAPA

UONGOZI wa Yanga umebainisha kuwa wana imani ya kushinda mbele ya Simba kwenye mchezo wao ujao wa Kombe la Shirikisho unaotarajiwa kuchezwa Kigoma, Julai 25.
Yanga imbainisha kuwa kwa namna ambavyo imejipanga haina mashaka na mchezo huo wa muhimu kwao kutwaa taji la FA ambalo lipo mikononi mwa Simba iliyotwaa msimu uliopita baada ya kushinda kwenye fainali mbele ya Namungo FC.
Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli amesema kuwa watakwenda Kigoma kwa namna ya kitofauti wakiwa na imani ya kutwaa taji la Shirikisho.
“Ikiwa wameshindwa kutufunga Uwanja wa Mkapa wakiwa na wachezaji wao wote wanaowataja kuwa ni bora unadhani wataweza kutufunga Kigoma?
“Hamna namna imani yetu ni kwamba wachezaji wao ambao watakuja uwanjani ni walewale na hakuna wa kuwaongeza kwa sasa ama unadhani watakuwepo wengine zaidi ya wale ambao tuliwafunga kwa Mkapa?
Kwenye msimamo Yanga ipo nafasi ya pili ikiwa na pointi 70 ilishinda mchezo wao wa ligi dhidi ya Simba Julai 3 kwa ushindi wa bao 1-0 lilifungwa na Zawad Mauya.
Simba ipo nafasi ya kwanza ikiwa imekusanya pointi 76 inahitaji pointi moja ili iweze kutangazwa kuwa bingwa rasmi kwa sasa na Bodi ya Ligi Tanzania Bara kwa kuwa pointi zake 76 ilizonazo kwa sasa zinaweza kufikiwa na Yanga ikishinda mechi zake mbili.
Kwenye mchezo huo uliochezwa Uwanja wa Mkapa miongoni mwa nyota wa Simba ambao walianza kikosi cha kwanza ni pamoja na Clatous Chama, Luis Miquissone na Bernard Morrison.

SOMA NA HII  MAPYA YAIBUKA...YANGA SC VS TP MAZEMBE...GSM AMALIZA MECHI MAPEMAA