BAADA ya kupata ushindi leo katika mchezo wa Ligi Kuu Bara mbele ya Geita Gold, Nasreddine Nabi Kocha Mkuu wa Yanga amesema kuwa watafanyia kazi tatizo la safu ya ushambuliaji kwa kuwa leo licha ya kushinda bao 1-0 ilipaswa kufunga mabao mengi.
Aidha ameweka wazi kuwa kwa sasa ligi ipo mwanzo mabadiliko yatakuwa yanaonekana taratibu huku akiamini kwamba kambi ya Arusha itawafanya waweze kuwa imara zaidi kwa kuwa watakaa pamoja muda mrefu.