Home news PAMOJA NA TIMU KUPATA MATOKEO…MGUNDA AVUNJA UKIMYA SIMBA…AANIKA ANACHOKITAKA ILI AFANYE KAZI...

PAMOJA NA TIMU KUPATA MATOKEO…MGUNDA AVUNJA UKIMYA SIMBA…AANIKA ANACHOKITAKA ILI AFANYE KAZI VIZURI…

Kocha wa Simba Juma Ramadhan Mgunda amewaomba mashabiki wa klabu hiyo kuendelea kumuombea kwa Mungu ili kazi yake ya kuifikisha klabu hiyo mahali fulani inafanikiwa na kuwapa furaha ambayo wanahitaji.

Mgunda alisema anashukuru kwa upendo ambao wanampa tangu amefika kwenye klabu hiyo na yeye anawapenda zaidi na akiwataka kuwa wasichoke kuisapoti na kuipenda timu yao kwenye kila nyakati ambayo itakuwa inapita.

Mgunda alisema: “Najua na ninaona upendo wa mashabiki wa Simba kwangu. Nafurahi na kufarijika sana kwa kila kitu ambacho wananionyesha. Nisema wazi kuwa hata mimi nawapenda sana.

“Kikubwa waendelee kuniombea kwa sababu kazi hii siyo rahisi, dua zao ndiyo nguzo yangu na timu yao. Jambo lingine la muhimu zaidi ni kwamba wasichoke kuja uwanjani hata kidogo, wachezaji wanawahitaji sana.”

Mgunda ameiongoza Simba kwenye mechi tano za kimashindano na kushinda zote na mechi zingine mbili za kirafiki nazo akifanikiwa kuiongoza Simba kwenye ushindi.

SOMA NA HII  KUHUSU KUCHEZA NNJE YA NCHI...MANULA AVUNJA UKIMYA...ATAJA CHANGAMOTO ANAYOPITIA...