MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu inatarajia kutoa hukumu ya kesi inayomkabili rais wa zamani wa Simba, Evans Aveva na makamu wake Geofrey Nyange Kaburu Oktoba 21 mwaka huu.
Kesi hiyo iliyo chini ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba jana hukumu yake iliahirishwa baada ya Kaburu kuiieleza Mahakama kuwa Aveva yupo klinic kutokana na kuumwa.
Katika kesi hiyo upande wa mashitaka ulikuwa na jumla ya mashahidi 10 na vielelezo mbalimbali huku washitakiwa wakijitetea wenyewe.
Mbali na Aveva washitakiwa wengine katika kesi hiyo ni Godfrey Nyange,(Kaburu) aliyekuwa makamu rais pamoja na Zachariah Hans Pope, ambaye ni marehemu.
Awali, mahakama hiyo iliwaona washitakiwa hao wana kesi ya kujibu katika mashtaka manne kati ya tisa yaliyokuwa yakiwakabili.
Mashtaka hayo ni pamoja na kula njama,kughushi, kuwasilisha nyaraka za kughushi na kutoa maelezo ya uongo.
Katika shitaka la kughushi linawakabili washtakiwa wote wanadaiwa walighushi hati ya malipo ya kibiashara ya Mei 28,2016 wakionesha kwamba nyasi bandia zilizonunuliwa na Simba zina thamani ya dola 40,577 sawa na zaidi ya milioni 90 za Tanzania huku wakijua kwamba siyo kweli.
Pia katika mashitaka mengine inadaiwa Aveva, Nyange na Hans Poppe kati ya Machi 10 na Septemba 30,2016 waliwasilisha nyaraka za uongo kuonyesha kuwa Simba imenunua nyasi bandia zenye thamani ya dola za kimarekani 40,577