Home news KIPA WA YANGA DIARRA AINGIA KWENYE VITA NA MANULA

KIPA WA YANGA DIARRA AINGIA KWENYE VITA NA MANULA


BAADA ya kutesa kwa takribani misimu sita kwenye Ligi Kuu Bara akifanikiwa kutwaa tuzo sita za kipa bora wa ligi hiyo, rasmi kipa wa Simba, Aishi Manula ameingia kwenye vita ya ufalme na kipa namba moja wa Yanga, Djigui Diarra aliyeanza vizuri.

Manula aliibuka kinara wa clean sheet, (Cheza bila kufungwa) msimu uliopita kwenye Ligi Kuu Bara, akifanikiwa kuwa nazo 18.

Msimu huu ambapo Simba na Yanga kila moja imecheza mechi mbili ndani ya Ligi Kuu Bara, Manula na Diarra kila mmoja ana clean sheet mbili.

Manula alikusanya clean sheet hizo dhidi ya Biashara United katika mchezo uliomalizika kwa suluhu na clean sheet ya pili aliipata dhidi ya Dodoma Jiji wakati Simba ikishinda 1-0.

Kwa upande wa Diarra, clean sheet ya kwanza aliipata dhidi ya Kagera Sugar, Yanga iliposhinda 1-0, huku ya pili akiipata dhidi ya Geita Gold, wakati Yanga ikishinda 1-0.

Kwa kuwa ni mwanzo wa msimu na ligi inaendelea ni suala la kusubiri na kuona nani ambaye atakuwa nani kwa kuwa kila timu inahitaji ushindi.

SOMA NA HII  KIPIGO CHA 4-0 KUTOKA BRIGHTON CHAWAINUA MASHABIKI MAN UTD...WIBUKA NA MSIMAMO HUU MKALI KWA WENYE TIMU...